Mayomboni

Mayomboni ni kata ya Wilaya ya Mkinga katika Mkoa wa Tanga, Tanzania.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 5,610 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,001 [2] waishio humo.

Mayomboni ni kata ya kaskazini-mashariki kabisa ya Tanzania ikiwa kwenye ufuko wa Bahari Hindi pale ambako mpaka wa Kenya na Tanzania inafika baharini.

Zamani barabara kuu ya Mombasa - Tanga ilipita hapa na kuvuka mpaka kwenye kijiji cha Yasini.

Wakati wa ukoloni wa Kijerumani kulikuwa hapa kituo cha forodha.

Kwenye Januari 1915 yalitokea hapa mapigano ya Yasini kati ya jeshi la Schutztruppe ya Kjerumani na jeshi la Kihindi-Kiingereza.

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Tanga - Mkinga DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-16.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search